Wednesday, October 24, 2012

Saturday, September 8, 2012

MITINDO HURU (FREESTYLE)

Freestyling

Mitindo huru ni moja kati ya nguzo za hip hop. Katika mitindo huru, mchenguaji (emcee) hua anaghani mashairi bila midundo ya ala ( instrumental beats),  au anaweza kughani kwa midundo. Mara nyingi mashairi anayoghani hua hayajatungwa kabla ya kufanya mtindo huru, (kwa lugha nyingine yanatoka kichwani). Kwenye zama za old school miaka ya 1980 hivi, neno mitindo huru lilimaanisha beti za mashairi yaliyoandikwa kabla ambayo hayazungumzii kitu chochote cha maana, ila lengo lake ni kuonyesha umahiri wa uandishi wa mashairi wa mtunzi husika. Kwenye kitabu cha How To Rap, Big Daddy Kane anasema, ‘'In the ’80s when we said we wrote a freestyle rap, that meant that it was a rhyme that you wrote that was free of style… it’s basically a rhyme just bragging about yourself.” Kulingana na maelezo ya Big Daddy Kane, inaonyesha kuwa mitindo huru ilihusu zaidi kujisifu kwa mchenguaji. Matumizi ya mistari konde (punchlines), sitiari (metaphor) na tashbihishi (similes) humuongezea sifa mchenguaji hasa katika mpambano wa mitindo huru.

Mitindo huru inaweza kufanyika kwa njia ya
1.Acapella,
2 Mitindo huru juu ya beatbox, yani mchenguaji anakua anachana huku mtu mwingine ana-beatbox, mfano kwenye mitindo huru mingi ya The Roots, Questlove hua ana-beatbox alafu Black Thought anaghani.
3.Kwa kutumia ala za midundo ya nyimbo za hip hop. Hii mara nyingi hitumika kwenye battles
4.Kufanya mitindohuru kama kundi la wasanii (cypher).
Katika kitabu chake cha There’s A God On The Mic, Kool Moe Dee anasema, "There are two types of freestyle. There’s an old-school freestyle that’s basically rhymes that you’ve written that may not have anything to do with any subject or that goes all over the place. Then there’s freestyle where you come off the top of the head'' Kulingana na maelezo ya Kool Moe Dee, Kuna aina mbili za mitindo huru,

 

1.MITINDO HURU ILIYOANDIKWA HAPO KABLA

 Pasipo kuathiri tafsiri yake ya awali ya mitindo huru, (Mitindo huru ni mashairi yaliyoandikwa hapo kabla ambayo hayahusu kitu chochote cha maana) Kool Moe Dee anatoa mifano ya nyimbo mbili ambazo zimeghaniwa kwa mfumo huu wa mitindo huru, Men at work ya Kool G Rap na Lyrics at fury ya Rakim,
  

2.MITINDO HURU AMBAYO HAIJAANDIKWA HAPO KABLA.

Mitindo huru inayotoka kichwani papo hapo, ambayo haikuandikwa hapo kabla.  Aina hii ya pili hutumika zaidi kwenye mpambano wa mtindo huru (freestyles battles), kuna wachenguaji mahiri ambao wanasifika kwa aina hii ya pili, mfano Canibus.

TAFSIRI MPYA

Katika documentary ya Kevin Fitzgerald, Freestyle: The Art Of Rhyme  anasema kuwa neno mitindo huru linavyotumika siku hizi hua lina maana moja tu, kughani mashairi ambayo hayakuandikwa hapo awali. Kool Moe Dee anasema, "A lot of the old-school artists didn’t even respect what’s being called freestyle now... any emcee coming off the top of the head wasn’t really respected. The sentiment was emcees only did that if they couldn’t write. The coming off the top of the head rhymer had a built-in excuse to not be critiqued as hard’’ Wasanii wengi wa zamani wanaona kama mitindo huru ya siku hizi haina maana maana wanaghani kila kitu kinachotoka kichwani, mfano, matusi, sifa za kijinga, nk.

FAIDA ZA MITINDO HURU

1.Burudani kwa mashabiki, hasa wakati wa tamasha
2.Kutafuta wasanii wenye vipaji vya kughani, kuna mifano ya wasanii wengi tu ambao wametoka kimuziki kupitia mashindano ya mitindo huru,
3.Kufunika makosa yako ya kiusanii katika nyimbo zako zilizopita. Mfano msanii akitoa nyimbo ya hovyo, mashabiki waka-diss, halafu kwenye tamasha akafanya mtindo huru mzuri, hii itamsaidia kufunika makosa yake ya nyuma.